Saturday, January 5, 2013

500,000Tsh Yanunua Ndege Tatu za Serikali.

WAZIRI wa Kilimo , Chakula na Ushirika , Mhandisi Christopher Chiza juzi  (4/1/2013) alishikwa na butwaa , pale alipopewa taarifa ya kuuzwa ndege tatu za Serikali , ambazo zilikuwa katika Kituo cha Kilimo Anga kwa kiasi cha Sh500,000 kwa kila moja . Ndege hizo, tatu zilikuwa zikitumika katika udhibiti wa wadudu waharibifu wa mazao . Akisoma taarifa ya kituo hicho mbele ya Waziri Chiza , Mhandisi Mkuu wa kituo hicho, Gideon Mugusi, alizitaja ndege hizo kuwa ni 5H-MRN, Cessna 185 nyingine ni 5H-MRF, Cessna 185 na nyingine aina ya 5H - MRP piper Super Cub ambazo zilianguka katika vipindi tofauti.
" Ndege zote tatu ziliharibika lakini Shirika la Bima la Taifa (NIC), walilipa Serikali kupitia katibu mkuu wa Wizaa ya Kilimo, kulingana na viwango vya bima vilivyo kuwa vikilipwa na wizara" alisema Mugusi. Hata hivyo alisema tangu kuanguka na kuuzwa kwa ndege hizo , shughuli za kituo hicho, zimekuwa zikidorora kwani marubani karibu wote wameondoka na kituo kimebaki na ndege moja tu ambayo pia ni mbovu na kibali chakuruka angani kimekwisha . Alisema kuwa sasa kutokana nakukosekana kwa ndege , gharama za uendeshaji wa shughuliza kituoni zimekuwa ni kubwa mno kwani wanalazimika kukodisha helikopta na gharama zake zimekuwa zikipanda mwaka hadi mwaka.

Source: JamiiForum.com