TOKA KERIO.
Maporomoko ya ardhi yaliyotokea katika eneo la
bonde la Kerio, magharibi mwa Kenya, jana usiku yamesababisha vifo vya Watu wanane baada ya
nyumba kadha kufukiwa.
Maporomoko hayo ya ardhi
yamesababishwa na mvua kubwa zilizonyesha katika bonde hilo.
Eneo la Kerio pia limekumbwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa inayonyesha.
Chama cha Msalaba Mwekundu cha Kenya kinasaidia jitihada za uokoaji na kutoa taarifa kwamba miili miwili ya watu wanane imeonekana na watu wengine watano waliokolewa
mapema leo. Watu wengi hawana makaazi kutokana na nyumba zao kusombwa na maji au kufukiwa na maporomoko ya ardhi.
