Monday, December 31, 2012

MAANDAMANO MAKUBWA AGAINST UBAKAJI INDIA

"Kwa kweli wanawake wengi nchini India wanakabiliwa na kitisho katika maisha yao katika mambo mbalimbali kama vile kunapozuka ghasia, ukosefu wa huduma za afya, kukosekana kwa usawa, kupuuzwa, lishe duni, kutojaliwa kwa afya ya mtu na utu wake"

Maelfu ya watu wamejiunga katika maandamano ya AMANI katika mji mkuu wa India, Delhi, kupinga kitendo kilichosababisha KIFO cha mwanamke mmoja mwenye miaka 23, ambaye alibakwa na kundi la wanaume mjini humo. Mwanamke huyo licha ya bado hajatambuliwa, amekufa kutokana na na majeraha Jumamosi huko Singapore alikopelekwa kupata matibabu maalum.
Wanaume sita wanashikiliwa kuhusiana na tukio la kumbaka mwanamke huyo, sasa wamefunguliwa mashitaka ya mauaji.
Shambulio hilo la aibu lilifanyika tarehe 16 Desemba 2012 na kusababisha maandamano kupinga unyanyasaji wanaofanyiwa wanawake nchini India.

Source: BBC Swahili.