MUNGU AILAZE PAHALI PEMA PEPONI
Mwanamuziki mkongwe katika Taarab Fatuma Bint Mbaraka maarufu kwa jina
la Bi Kidude alifariki dunia jana mchana, 17/4 huko Bububu
Zanzibar, sehemu alikokuwa anaugulia kwa kipindi sasa.
Bi Kidude
alizaliwa katika kijiji cha Mfagimaringo..Alikuwa binti... wa mchuuzi wa
nazi na hakuna anayejua haswa Bibi huyu alizaliwa tarehe ngapi, kuna hata
mawazo kuwa alikwishafikisha miaka 102.
Katika mwaka 1920 tayari alikuwa amekwisha anza kuimba katika vikundi
vya sanaa kule kwao...mwaka 1930 alijiunga na Egyptian Musical Club ya
Dar es Salaam na kuzunguka miji mingi ya Tanganyika wakati ule .....
Mwaka
1940 alirudi Zanzibar ambako awali alikuwa amekimbia kwa kuwa aliozwa
kwa nguvu na mtu aliyemzidi sana umri.
Bi Kidude pia aliwahi kuimba na Sitti Binti Sadi wakati wa ujana wake,
na katika maisha yake Bi Kidude amekwisha zunguka mabara yote akiimba
katika majukwaa na wanamuziki maarufu ulimwenguni
Na leo hii ndio imeshudiwa safari yake ya mwisho.
Mungu Amlaze Pema Peponi Bibi yetu. Amen