WACHEZAJI wa Yanga waliwasili Uturuki siku ya Jumapili na mara moja walianza mazoezi makali mithili ya yale kijeshi huku wakipigwa mvua na baridi kali katika viwanja vya Fame Residence hapa Antalya, Uturuki.
Yanga ilianza mazoezi Chini ya kocha wao Ernie Brandts, siku ya Jumatatu asubuhi ambapo licha kukuta hali ya mvua na baridi, hiyo haikuwa kikwazo kabisa kwao. Didier Kavumbagu pekee ndie hakushuka mazoezini. Kavumbagu anakabiliwa na maumivu ya enka.
Kwa mujibu wa gazeti la Mwanaspoti, imelipotiwa wachezaki hao wa Yanga wako katika mazoezi mazito yanayolinganishwa na yale ya 'kijeshi'. Brandts alihakikisha anawafanyisha mazoezi makali ya viungo na kuwakimbiza ili miili yao ichemke kutokana baridi kali ya Uturuki pia lengo kubwa ikiwa kuwazoeza na hali ya hewa.
Mwanaspoti lilipoti ''Aliwapa mazoezi yanayoogopewa mara zote yakiwa na sura halisi ya kijeshi. Mazoezi hayo kihistoria yalianza mwaka 1740 katika Dola ya zamani ya Prussia huko barani Ulaya (Sasa Ujerumani). Wachezaji wa Yanga wana kibarua cha kujizoeza na hali ya hewa ya hapa kwani wametokea Dar es Salaam ambako kuna joto kali.''
Yanga imeweka kambi yake katika mji wa Antalya ambako ni mwendo wa dakika 50 kwa ndege kutoka mji mkuu wa Uturuki, Istanbul. Naye Kocha wa makipa ameripoti kupitia mtandao wa klabu yakua mazingira ya kambi ni ya kuridhisha, vifaa vya mazoezi vipo kwa wingi hivyo kurahisisha kazi yao walimu.
Yanga iliwasili Uturuki Jumapili, na mazoezi yanaedelea vizuri wakiwa na hawamu mbili ya mchana na jioni, lengo kuu ni kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

