![]() |
| Walcott akielekea katika lango la Newcastle, |
Arsenal yairarua New Castle 7-3
Arsenal imeiangushia kipigo kikali New Castle kwa kuicharaza magoli 7-3 katika mchezo wa ligi kuu ya England uliofanyika Jumamosi kwenye uwanja wa Emirates.Theo Walcott alikuwa mwiba katika ngome ya New Castle baada ya kuibuka na magoli matatu kati ya saba yaliyofungwa na Arsenal, Jumamosi katika mchezo uliofanyika uwanja wa Emirates. Walcott pia alichangia upatikanaji wa magoli mawili zaidi kwa kutoa pasi nzuri kwa wafungaji. Kwa matokeo hayo Arsenal imepanda hadi nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kuu ya England.
![]() |
| Robin Van Persie akisherehekea bao lake |
Man United yaendeleza ushindi wao
Manchester United jana (j'mosi) imeilaza West Brom magoli 2-0 na kujihakikishia nafasi ya kwanza kwenye msururu wa ligi kuu ya Premier ya England, mwanzo wa mwaka ujao wa 2013.Gareth McAuley alijifunga mwenye na kuipa Manchester United, bao lao la kwanza kabla ya Robin Van Persie kufunga bao la pili.
Baada ya mechi ishirini Mancheter United, inaongoza msururu wa ligi na alama 49, alama saba mbele ya mabingwa watetezi Manchester City.
Pos Club (Games played & Points)
1 Manchester United 20 - 49
2 Manchester City 20 - 42
3 Tottenham Hotspur 20 - 36
4 Chelsea 18 - 35
5 Arsenal 19 - 33
6 Everton 19 - 33
7 W.B Albion 20 - 33
8 Stoke City 20 - 29
9 Swansea City 20 - 28
10 Liverpool 19 - 25
11 Norwich City 20 - 25
12 West Ham United 19 - 23
13 Sunderland 20 - 22
14 Fulham 20 - 21
15 Newcastle United 20 - 20
16 Wigan Athletic 20 - 18
17 Aston Villa 20 - 18
18 Southampton 19 - 17
19 Reading 20 - 13
20 Q.P Rangers 19 - 10


