Frank
Lampard, Miaka 34, ambae mwishoni mwa Msimu Mkataba wake unamalizika na
inadaiwa tayari hana nafasi Klabu hapo, leo alivaa utepe wa Nahodha na kuibeba
Chelsea toka Goli 1 nyuma Uwanjani Goodison Park na yeye mwenyewe kupiga Bao
mbili na kuwapa ushindi wa Bao 2-1, ukiwa ni ushindi wao wa kwanza kwa Miaka
minne Uwanjani hapo.
Hi ilikuwa ni Mechi ya mwisho ya Ligi Kuu England
kwa Mwaka 2012 kwa Klabu zote mbili ambazo zitacheza Mechi zao za Ligi
zinazofuata hapo Januari 2, Mwaka 2013 kwa Chelsea kuikaribisha QPR Uwanjani
Stamford Bridge na Everton kuwa ugenini huko St James Park kuivaa Newcastle
Goli la Everton lilifungwa na Pienaar
Dakika ya 2, wakati magoli ya Chelsea FC yote mawili yakifungwa na Lampard
Dakika ya 42 & 72.
Ushindi huu wa leo umeipaisha Chelsea kukamata
nafasi ya 3 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Timu ya Pili Manchester City huku wao
wakiwa na Mechi moja mkononi.
Tofauti ya Magoli inatajwa kwa Timu zilizofungana
Pointi
1 Man United Mechi 20 Pointi 492 Man City Mechi 20 Pointi 42
3 Chelsea Mechi 19 Pointi 38
4 Tottenham Mechi 20 Pointi 36
5 Arsenal Mechi 19 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli
18]
6 Everton Mechi 20 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli
8]7 WBA Mechi 20 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 3]
8 Stoke Mechi 20 Pointi 29
9 Swansea Mechi 20 Pointi 28
10 Liverpool Mechi 19 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli 2]

