Wednesday, July 4, 2012

Wajerumani kuchukua hatua

Wasimamizi wakuu wa
televisheni nchini Ujerumani
wamesema watawasilisha
malalamiko yao rasmi kwa
wakuu wa soka barani Ulaya,
kufuatia picha za shabiki mmoja aliyetokwa na machozi
zikionyeshwa, mara tu baada
ya Italia kufunga goli la pili
katika michuano ya Euro 2012
katika mechi ya nusu fainali
dhidi ya Ujerumani. Shabiki huyo, ambaye ni
mwanamke, alikuwa amejipaka
rangi zilizomo katika bendera
ya Ujerumani, na alielezea
kwamba alitokwa na machezo
wakati timu ya Ujerumani ilipokuwa ikiingia uwanjani, na
wala sio baada ya timu hiyo
kufungwa. Anasema alitokwa na machozi
kwa msisimko wa kuwatizama
wachezaji wa timu ya
nyumbani. Hii ndio pia Wajerumani wengi
waliitizama wakiwa nyumbani. Wakati Ujerumani ilipoingia
katika mashindano hayo, ndio
timu iliyotazamiwa na wengi
kupata ushindi, na kinyume na
hayo, picha walioitizama ya
mwanamke kijana akibubujikwa na machozi, na
aliyejipaka rangi za bendera ya
Ujerumani, nyekundu, manjano
na nyeusi, ni jambo ambalo
liliwaudhi mashabiki wengi wa
Ujerumani. Suala muhimu hapa ni kwamba
mambo hayakuwa hivyo. Picha hiyo ilitumiwa wakati wa
kuonyesha matangazo ya moja
kwa moja, na wengi
wakadhani mwanamke huyo
alikuwa akilia wakati huo. Hiyo haikuwa mara ya kwanza. Mapema katika michuano hiyo,
kocha wa Ujerumani, Joachim
Loew, alionekana akifanya
utani na kijana mmoja wa
kukimbilia mipira uwanjani,
huku akionekana kufurahi, na timu yake ikiendelea
kupambana uwanjani, na
haikueleweka kwa nini alikuwa
akitabasamu na kufurahia
hayo. Picha hiyo ilikuwa imepigwa
wakati wa mazoezi, na kisha
kutumiwa katika matangazo ya
moja kwa moja. Sasa wanaosimamia matangazo
ya televisheni nchini Ujerumani
wanasema matangazo ya moja
kwa moja lazima yawe hivyo,
na pasipo udanganyifu kwa
kutumia picha zilizonaswa mapema.

(Source: BBC Swahili)