Kwa mara ya kwanza kifaa cha
kujipima iwapo mtu ana virusi
vinavyosababisha ukimwi
kimeidhinishwa na wataalam
wanaodhibiti sekta ya Afya nchini
Marekani. Kifaa hicho kwa jina OraQuick
kitawezesha watu kutumia mate
kuchunguza kama wana virusi vya
ukimwi. Itachukua muda wa kati ya dakika 20
na 40 kubaini matokeo ya uchunguzi
huo. Kifaa hicho ambacho kitawezesha mtu
kuchunguza hali yake mwenyewe
nyumbani au kokote anakotaka
kitaanza kuuzwa nchini Marekani
mwezi Oktoba mwaka huu. Serikali ya Marekani inatarajia kuwa
kifaa hicho kitasaidia kupunguza
maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa
kubadili tabia miongoni mwa watu
wanaoishi na virusi bila kujua. Inakadiriwa kuwa robo millioni ya
Wamarekani wako katika kitengo
hicho. Utafiti wa kimatibabu unaoyesha
kuwa majaribio ya matokeo ya
uchunguzi wa kifaa hicho cha
Oraquick yananaweza kuwa sahihi
kwa asilimia tisini na mbili, miongoni
mwa watu wanoishi na virusi vya ukimwi.
(Source: BBC Swahili)
