| Chadema kuwaaga waliouawa Januari 12 uwanja wa NMC | Send to a friend |
| Sunday, 09 January 2011 20:57 |
0diggsdigg Moses Mashalla, ArushaUONGOZI wa Chadema umetangaza Januari 12, mwaka huu, itakuwa siku ya kuaga watu wote waliouwa kwa kupigwa na risasi na polisi kwenye maandamano jijini Arusha. Chadema kilisema siku hiyo ndugu, jamaa, marafiki na wanachama wa chama hicho, watatoa heshima zao za mwisho kwenye uwanja wa NMC. Tamko hilo lilitolewa juzi na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alipotembelea familia za waliouwa kwenye maandamano ya amani ya chama hicho mkoani hapa. Mbowe, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro, alisema uongozi wa chama unafanya jitihada za kuwaaga kwa pamoja, marehemu ambao aliwaita mashujaa wa kweli. Akiongozana na Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini, Godbless Lema, viongozi wa chama mkoani hapa na wabunge wa viti maalumu, alisema lengo ni kutoa fursa kwa wananchi wote, wakiwamo wafuasi wa chama hicho nchini kuwaaga marehemu hao kwa pamoja. Huku Mbowe akionyesha mojawapo ya ganda la risasi aliyotumika na polisi kuua raia, alisema marehemu waliouawa na polisi kwenye harakati za kudai haki liyoporwa muda mrefu, hivyo wanastahili kupewa heshima yao. “Jamani haki haiombwi, haki inatafutwa, hawa waliokufa ni mashujaa wa kweli, hivyo tunapanga kuwapa fursa wafuasi wote wa Chadema na wananchi kwa pamoja, ili tuwaage marehemu eneo la NMC,” alisema Mbowe. Hata hivyo, Mbowe alisema chama chao bado kinafanya juhudi za kufuatilia maiti mbili zilizopelekwa Hospitali ya Rufani KCMC, usiku wa tukio wakiwa na risasi mwilini. Naye Lema alishutumu polisi nchini kwa kutumia risasi kuua raia badala ya kulinda usalama wao na kwamba, moto uliowashwa kamwe hautazimika. Akizungumza kwa hisia, Lema alisema kitendo cha kuwafyatulia risasi na kuwaua wananchi ni unyama uliovuka mipaka, kwani wengine siku hiyo walikuwa wakisaka mkate wao, hawakuhusika na maandamano hayo. |