Kuelekea pambano la leo kati ya Bondia Bingwa hapa nchini Tanzania kuvaana na bondia Chiotcha Chimwemwe toka Malawi, Mfalme wa michano, King Afande Sele ametoa sapoti na kuwasihi mashabiki wazalendo kumiminika kwa wingi pale kiwanjani Jamhuri kushuhudia pambano hio la kukatana shoka.
Katika ukurasa wake nguli huyo wa Rymes ameandika "...dua zenu ni mhmu
sana wana'ndugu kwa kuwa kusema ukweli siku
zote mimi huwa sina mashaka na mechi zote za
mdogo wangu francis kwa kuwa daima namuamini
sana lkn leo nakwenda jamhuri huku nikijua wazi
mchezo ni mgumu lkn...."
REKODI YAKE CHEKA:
Kashinda mara 28 (KO 16)
Kapoteza mara 7 (KO 4)
Suluhu 1
Cheka ni Bondia namba moja hapa nchini,
Na amewatoa hofu mashabiki wake na kusema amejipanga kumchapa mpinzani wake, Chiotcha Chimwemwe kutoka Malawi leo hii.
"Ni lazima nishinde ili kulinda heshima yangu, najua litakuwa pambano gumu lakini Chimwemwe hawezi kunipiga," alisema Cheka.
Jioni hii Cheka na Chimwemwe wanamaliza ubishi wa nani mkali baina yao kwenye Uwanja wa Jamhuri katika pambano la uzani wa 'Super Middle' raundi nane.
Katika zoezi la kupima uzito, Chimwemwe alikuwa na kilo 73, huku Cheka akiwa na kilo 75, uzito ambao Chama cha Ngumi za Kulipwa cha PST kimeeleza hauna tatizo.
Pambano la leo litakuwa la pili kuwakutanisha
Cheka na Chimwemwe, ambapo pambano la
kwanza Cheka alishinda kwa pointi za majaji 2-1 mwaka jana jijini Arusha.
Bondia Francis Cheka ni mzaliwa wa Dar es Salaam na makazi yake ni mkoani Morogoro.