Saturday, April 20, 2013

VICE PRESIDENT MPYA WA MAYBACH MUSIC GROUP [MMG]

Kedell Freeman
Bosi wa 'kru' ya MMG, Rick Ross, amemchagua rasmi mnyamwezi Kendell Freeman p.k.a. Young Sav kuwa kama msaidizi wake - Vice Persident wa lebo yake ya MMG. Mkali huyu amekuwa na mchango mkubwa sana katika muziki wa Rick Ross, na katika profile yake, amekwishapiga kazi ya nguvu na wakali kama vile Lil' Jon, Pitbull, na Ying Yang Twins, Young Sav pia akiwa chini ya lebo ya Def Jam kama Mixshow Manager, amepata nafasi ya kufanya kazi kwa karibu na Jay-Z akiwepo pia Rick Ross, 2 Chainz, Fabolous na Jadakiss.
Ross amesema anajisikia poa sana kuwa na mtu kama Young Sav ndani ya Maybach Music Group, na kwa upande wake the new Vice President Amemshukuru sana Ross kwa kuona jitihada zake na kumuweka katika nafasi kubwa kama hii.