Kati ya
picha zilizo make headline sana za celebs wakisherehekea sikukuu ya Christmas,
picha za Rihanna na Chris Brown zilisambaa sana na kuwa gumzo. Chris Brown
ambae anamahusiano yenye drama na warembo wawili Karruache Tran na
Rihanna anaendelea kuwaumiza vichwa.
Siku ya
Christmas Chris Brown alienda kuangalia game la Lakers na Rihanna,
na kwa mujibu wa watu wa karibu sana wa Karruache Tran ni kwamba Chris
Brown alikuwa ameshamwambia kuwa atatoka na Rihanna siku hiyo ya
Christmas tena wiki moja kabla.
Hii
ilionekana kumuumiza mrembo huyo lakini alivumilia tu kwa sababu alikuwa
anachat na Chris Brown wakati wanaangalia mpira wa kikapu na Rihanna
huko Los Angeles. Lakini hasira zilimzidia baada ya habari kuwekwa wazi kuwa Chris
na Rihanna walilala pamoja usiku huo wa Christmas, na December 27,
aliweka wazi hisia zake kwenye mtandao wa kijamii wa twitter kwa tweet yake
ambayo ilikuwa imewekwa kimafumbo lakini inaonekana kabisa kuwa ilielekezwa kwa
Chris Brown na Rihanna.
Tweet
yake ilisomeka, “Wishing death upon someone is some weak s**t.”
Hii inaonesha hisia kali alizonazo Karruache ambapo inawezekana kabisa
kuwa hakua na nia ya moja kwa moja ya kumuombea mtu kifo kama inavyoonekana,
kwa sababu ni kitendo cha kinyonge na cha kipuuzi, lakini inaonesha jinsi gani
alichukizwa na kitendo cha wa wawili hao kujiachia hadharani na kumdhalilisha
yeye kiivo.
Hii ni
kama inazunguka hivi ama tuseme ingekuwa enzi zile tungeita ‘kutesa kwa zamu’
kwa sababu hivi karibuni Karrueche alipokuwa na Chris Brown huko Paris,
Rihanna alionekana kuumia sana na kumshambulia Chris kwenye
Twitter.
gossip from TMZ.com
gossip from TMZ.com

