Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, amezindua rasmi maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, leo yanayofanyika Kitaifa Mkoani Kilimanjaro.
Makamu wa Rais wa Dkt. Bilal, pia alipanda mti aina ya Mroliondo katika eneo la Chem chem ya Maji Njoro,leo ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayofanyika Kitaifa Mkoani Kilimanjaro.
Pia Makamu wa Raisi, Dkt.Bilal, aliwahutubia wananchi wa Mkoani Kilimanjaro, wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, leo Juni 03, 2012, ambayo yalifanyika Kitaifa Mkoani Kilimanjaro.



