MDAHALO WA BWIRU BOYS & MIHAMA FEMA CLUBS.
Katika kuendeleza harakati za uelimishaji ktk jamii, klabs za FEMA zimeonekana kutoa mchango mkubwa sana.
Mnamo tarehe 18/Mei/2012 klabu ya Bwiru Boys FEMA Club waliitembelea klabu ya Mihama Secondary FEMA Club shuleni kwao majira ya mchana na kupata mapokezi mazuri na kujumuika ktk mjadala wa pamoja.
Swala mezani likiwa ''Kwa Nini Wanafunzi Wanakatazwa Kujihusisha na Mapenzi?'', vijana walichangia mawazo kwa upana wao.
Miongoni wa yalipewa kipaumbele ni adhari za mwanafunzi kujihusisha na mapenzi shuleni na nje ya shule. Adhari hizo ni:
> Kupoteza muda na mwelekeo.
> Kupata mimba au kusababisha mimba.
> Kupata VVU/UKIMWI na magonjwa ya zinaa.
> Madhara ya kisaikolojia, n.k.
'Wanafunzi ni wanafunzi'.. katika kujitetea kwa upande wao (wanafunzi), walijaribu kuainisha Faida,uku mmoja akichangia kuwa Mapenzi yanasaidia kujuana mapema kati ya wapenzi,
Penye wengi hapakosi mambo. Misemo nayo ilichukua nafasi yake. ''Huwezi tumikia mabwana wawili (mapenzi & elimu)'', ''Mshika mawili moja humponyoka'', ''Unaweza fanywa spare tyre'', ''Unadhani mtu kumbe si kitu'' na juu ya yote burudani ni pale mchangiaji mmoja alipojaribu kutoa maana ya neno DEMU - Daima Epuka Mapenzi Utotoni.
Kama kawaiba FEMA ni kuelimika na kuburudika. Burudani mbalimbali zilikonga nyoyo za watu, lakini vijana hawa - Comedy Mtu Chee na kijana wa kushake, Kisako Shabani ndio walioshaniliwa sana.